Mkatoliki Imara

Karibu katika Facebook Page ya Mkatoliki Imara https://web.facebook.com/MkatolikiImara/ Mkatoliki Imara

SIKUKUU YA JINA TAKATIFU LA MARIA

September 12, 2019

 

Leo kanisa linaadhimisha sikukuu ya jina kuu la Mama yetu Maria.Mama Maria, ni mama wa mkombozi wetu, Bwana wetu Yesu Kristo.
Sherehe hizi zilianza mwaka 1513, kama Sherehe katika mji wa Cuenca, Hispania.
Mwaka 1587 Papa Sixtus V aliihamishia sikukuu hiyo tarehe 15 September, na mwaka 1622 Papa Gregory XV, aliidhinisha Sherehe hiyo kufanyika katika mji wa Toledo.

Na mwaka 1671 Sherehe ilifanyika nchi nzima ya Hispania. Ikasambaa mpaka Naples ,Italia.Papa Innocent XI aliiweka siku hii katika kalenda ya kanisa,na kuwa 12 September.
Na mwisho Papa John Paul II akaiimarisha katika kalenda ya kanisa, kwa tarehe hiyo hiyo ya September 12.

Watakatifu wengine wa leo ni
Mt. Ailbhe
Mt. Autonomous
Mt. Curomotus
Mt. Eanswida
Mt. Francis wa Mt. Bonaventure
Mt. Guy wa Anderlecht
Mt. Hieronides
Mt. Macedonius
M/h. Mancius wa Mt. Thomas
Mt. Peter Paul wa Mt. Claire
Mt. Sacerdos wa Lyon
M/h. Thomas Zumarraga


Mama Maria, mwombezi wetu, utuombee
Wenye heri na Watakatifu wengine wa leo, Mtuombee


Posted at: 08:03 PM | 0 Comments | Add Comment | Permalink

Posts by Date

Recent Posts

Archives